• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KRA YASEMA ITAENDELEA KUKUSANYA USHURU LICHA YA BUNGE KUFTA SHERIA 23.

    (GMT+08:00) 2020-11-02 16:58:08

    Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA) imefafanua kuwa itaendelea kukusanya ushuru kwa kutumia sheria zilizopitishwa na Bunge la Kitaifa pasi na kushirikishwa kwa Seneti.

    Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa ya wiki iliyopita, KRA ilisema kuwa ina muda wa miezi sita kuendelea kutumia sheria hizo, kipindi ambacho kilitolewa na mahakama kwa bunge la kitaifa kuhakikisha kuwa limetoa nafasi kwa mchango wa Seneti.

    Mnamo Alhamisi majaji watatu wa mahakama kuu walibatilisha sheria 23 zilizopitishwa na bunge la kitaifa mnamo 2018, ikiwemo Sheria ya Fedha ya 2018, bila mchango wa Seneti hatua ambayo walisema ni kinyume cha Katiba.

    Marekebisho ya sheria ya ushuru ya 2018 yaliyoanzisha hitaji kwamba wafanyabiashara wadogo kama mama mboga na wasusi kulipa ushuru wa kima asimilia 15 ya ada ya leseni za biashara ambazo hutolewa na serikali za kaunti pia imeathirika na uamuzi wa majaji hao watatu.

    Ushuru huo unaojulikana kwa kimombo kama "presumptive tax" ulitoa nafasi kwa KRA kukusanya data zaidi kuhusu wafanyabiashara wadogo na hivyo kutoa nafasi kwa kuanzishwa kwa ushuru unaotozwa faida za wafanyabiashara hao, almaarufu, "turnover tax"

    Sheria nyingine iliyoathirika na uamuzi huo wa Mahakama Kuu ni Sheria ya Marekebisho ya sheria za kitaifa za Afya ya 2018.

    Sheria hiyo iliipa Mamlaka ya Usambazaji Dawa na Vifaa vya Kimatibabu (Kemsa) ukiritimba wa kuziuzia serikali za kaunti dawa na vifaa vinginevyo vya kimatibabu. Serikali hizo zimekuwa zikilalamikia sheria hiyo zikisema zimezuiwa kununua dawa kutoka kwa kampuni zingine ilhali Kemsa huwauzia dawa kwa bei ghali mno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako