Habari kutoka shirika la habari la Reuters zinasema, kutokana na kuboreshwa kwa hali ya uchumi wa China, uchumi wa Asia umeanza kufufuka. China inaingia katika kipindi kipya cha ongezeko baada ya kuripoti watu wa kwanza walioambukizwa virusi vya Corona duniani karibu mwaka mmoja uliopita.
Baada ya kutekeleza zuio kali kabisa duniani mwanzoni mwa janga la COVID-19, sasa China ni nchi pekee ambayo ilikadiriwa na Shirika la Fedha Duniani kutimiza ongezeko la uchumi mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |