• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani haina haki ya kuwa "mwalimu wa haki za binadamu"

    (GMT+08:00) 2020-11-02 19:28:54

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, Marekani haina haki ya kujifanya kama "mwalimu wa haki za binadamu", na haipaswi kutengeneza virusi vya kisiasa na habari za uwongo.

    Wang amesema hayo kufuatia wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuanzisha tovuti kuhusu haki za binadamu nchini China, na kuilaani China kwa kutoheshimu haki za binadamu katika mambo ya Xinjiang, Tibet, Hongkong na shughuli za kidini.

    Amesema serikali ya China inazingatia maslahi ya wananchi wake, na kuwasaidia zaidi ya watu milioni 700 kuondokana na umaskini. Ameongeza kuwa China imekamilisha mifumo mikubwa zaidi duniani ya elimu, huduma za jamii, matibabu na demokrasia ya shina, na kulinda vizuri uhuru wa raia wa kuongea, kuamini, na watu wa makabila madogo kujiunga na utawala wa mambo ya kitaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako