• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa kwenye tetemeko la ardhi nchini Uturuki yafikia 79

    (GMT+08:00) 2020-11-02 19:29:22

    Takriban watu 79 wamefariki na wengine 962 kujeruhiwa kwenye tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Izmir uliopo magharibi mwa Uturuki.

    Kwenye taarifa yake Mamlaka ya Usimamizi wa Majanga na Dharura ya nchi hiyo AFAD, imesema operesheni ya uokozi bado inaendelea kwenye mabaki ya majengo manane yaliyoporomoka katika mkoa huo. Televisheni ya CNN tawi la Uturuki imetangaza moja kwa moja kwamba mtoto wa kike Elif Perincek mwenye umri wa miaka 3 aliokolewa chini ya mabaki hayo saa 65 baada ya tetemeko hilo lenye nguvu ya 6.6 kutokea mapema Ijumaa asubuhi.

    Naibu Meneja wa Brigedia ya ZimaMoto katika jiji la Istanbul Ahmet Yavuz ambaye anaongoza timu ya uokozi amesema waokoaji walipata tabu kumuokoa Elif kwa siku tatu na kutumia juhudi kubwa bila kusita. Kwa mujibu wa ripoti hadi sasa jumla ya watu 106 wamepatikana kwenye vifusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako