• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lori lavamia sokoni na kuua watu 16 kusini magharibi mwa Nigeria

    (GMT+08:00) 2020-11-02 19:29:59

    Takriban watu 16 wameuawa na wengine saba kujeruhiwa wakati lori lilipovamia sokoni Jumamosi kusini magharibi mwa Nigeria.

    Kwenye taarifa yake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani FRSC Boboye Oyeyemi amesema tukio hilo limetokea huko Akungba Akoko kwenye jimbo la Ondo. Amefafanua kuwa kati ya watu 23 waliohusika kwenye tukio hilo, watu saba wakiwemo wanaume watu wazima watatu, wanawake watu wazima watatu na mtoto mmoja waliokolewa wakiwa na majeraha ya kiwango tofauti na kupelekwa hospitali.

    Bado haijajulikana sababu ya lori hilo kuvamia sokoni lakini uendeshaji gari vibaya na barabara mbovu ni miongoni mwa sababu kubwa za ajali barabarani nchini Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako