• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana na SADC zawapongeza Watanzania kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura

    (GMT+08:00) 2020-11-02 19:30:52

    Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi jana aliwapongeza Watanzania kwa mara nyingine kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura.

    Masisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC amesema kwenye taarifa kwamba, Watanzania kwa mara nyingine tena wamepiga kura kwa amani na utulivu Oktoba 28, ikiashiria kuwepo kwa maendeleo yaliyotokana na chaguzi sita za vyama vingi tangu mwaka 1995.

    Kwa mujibu wa taarifa, SADC pia imewapongeza marais wateule John Pombe Magufuli wa Tanzania bara na Hussein Ali Mwinyi wa Tanzania Zanzibar kwa kushinda uchaguzi pamoja na vyama vya kisiasa na wagombea wengine, na kuwahamasisha kujumuisha mafanikio yaliyopatikana kwenye demokrasia tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi katika nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako