• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkurugenzi mkuu wa WHO ajitenga nyumbani kutokana na kuwa karibu na mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-11-03 08:53:37

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus jana kwenye ukurasa wake wa tovuti ya kijamii alisema, kutokana na kuwa karibu na mtu aliyeambukizwa virusi vya Corona, amejitenga nyumbani, lakini hana dalili yoyote ya ugonjwa.

    Dr. Tedros amesema ni muhimu kwa watu wote kufuata mwongozo wa afya, ambao ni njia ya kuzuia kusambaa na kuenea kwa virusi, na pia kulinda mfumo wa afya.

    Shirika la Afya Duniani jana limesema, matokeo ya vipimo vya virusi vya Corona ya Bw. Tedros yameonyesha hana maambukizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako