• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malipo kwa kupitia simu za mkononi kila siku nchini Kenya kutokana na janga la COVID-19 yaongezeka

    (GMT+08:00) 2020-11-03 09:01:16

    Malipo kwa kupitia simu za mkononi nchini Kenya yameongezeka na kufikia dola za kimarekani milioni 147 kwa siku kutokana na matumizi ya huduma hiyo kufikia kiwango cha juu, sehemu kubwa ikiwa inachangiwa na hatua zilizochukuliwa kupambana na virusi vya Corona.

    Serikali ya Kenya kupitia Benki Kuu ya nchi hiyo iliweka hatua kadhaa za kupambana na virusi vya Corona ambavyo vimeongeza matumizi ya huduma hiyo. Hatua hizo ni pamoja na kuondoa gharama za malipo yanayoanzia dola 9.25 za kimarekani na chini ya hapo kwa lengo la kupunguza matumizi ya pesa taslimu. Serikali hiyo pia iliongeza kiasi cha malipo kwa siku kutoka dola za kimarekani 1,388 hadi 2,777.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako