• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yazindua sherehe za vijana licha ya kuwepo kwa janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-11-03 09:01:38

    Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) imezindua Mwezi wa Vijana wa Afrika, sherehe za mwezi mzima zinazowalenga vijana wa Afrika wenye umri wa chini ya miaka 35, ambao wanachukua asilimia 75 ya wakazi wa Afrika wanaofikia bilioni 1.2.

    Katika ujumbe wake uliotolewa jana kuhusu sherehe hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema, mwaka huu sherehe hizo zinafanyika katika hali ya kipekee kutokana na janga la virusi vya Corona. Ametoa salamu maalum kwa wafanyakazi wote walioko mstari wa mbele, ambao wengi wao ni vijana, wanaojitahidi kuhakikisha usalama wa jamii na familia.

    Amesema vijana hao wanatumia uvumbuzi na ubunifu kusaidia kufuatilia virusi huku wakitoa elimu sahihi kwa jamii, kwa lugha zao, kuhusu jinsi ya kudumisha afya bora na kulinda ndugu na jamaa dhidi ya virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako