• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda azindua ilani ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2021

    (GMT+08:00) 2020-11-03 09:02:02

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezindua ilani yake ya uchaguzi ya miaka mitano kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani nchini humo.

    Rais Museveni, ambaye ni mgombea kutoka chama tawala cha NRM nchini humo, amesema ilani hiyo ya mwaka 2021-2025, chini ya kaulimbiu "Kuhakikisha hatma yako", inajikita katika vipaumbele vitano vinavyojumuisha kuunda ustawi na ajira, kutoa elimu na huduma za afya, kuhakikisha haki na usawa, ulinzi wa mali na maisha, na kutimiza mwingiliano wa uchumi na siasa.

    Rais Museveni amesema, vipaumbele vyake ni ulinzi, upatikanaji wa umeme, ujenzi wa barabara na reli, afya, elimu, na kuwalipa vizuri wanasayansi wa serikali.

    Amewataka Waganda kuendelea kuichagua NRM kuongoza nchi ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii nchini Uganda.

    Jana, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda alimtangaza rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, kuwa mgombea urais wa chama cha NRM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako