• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu zaidi ya saba wauawa kwenye shambulizi la risasi mjini Vienna

    (GMT+08:00) 2020-11-03 10:20:15

    Watu zaidi ya saba wameuawa akiwemo askari polisi mmoja na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la risasi lililotokea jana usiku karibu na kanisa moja huko Vienna, mji mkuu wa Austria.

    Vyombo vya habari nchini humo vimesema, watu kadhaa waliokuwa na bunduki walifanya shambulizi hilo, na mmoja wao amekamatwa na polisi wakati akitoroka. Hivi sasa polisi wamezunguka duka kubwa la manunuzi, na inaaminika kuwa huenda watu hao wanawashikilia mateka.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Austria Karl Nehammer amelitangaza shambulizi hilo kuwa ni la kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako