• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la maambukizi ya COVID-19 kwa siku nchini Marekani lafikia 80,000

    (GMT+08:00) 2020-11-03 10:20:45

    Takwimu zilizotolewa jana na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani zimeonyesha kuwa, Marekani imeweka rekodi mpya ya kesi za maambukizi wa virusi vya Corona kwa siku, ambazo zimefikia 80,000.

    Kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, hadi kufikia Jumatatu alasiri, watu zaidi ya milioni 9.26 walithibitishwa kuambukizwa COVID-19 nchini Marekani, na idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo nchini humo imefikia 231,300.

    Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza nchini Marekani Anthony Fauci amesema, nchi hiyo itakuwa na hali mbaya zaidi katika miezi ijayo kutokana na janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako