• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Guardiola asema muda wake Barcelona umekwisha

    (GMT+08:00) 2020-11-03 17:06:48

    Pep Guardiola anasisitiza kuwa muda wake katika klabu ya Barcelona umekwisha baada ya mkufunzi huyo wa Manchester City kuhusishwa na uhamisho wa kurudi katika mabingwa hao wa Uhispania. Mgombea wa wadhfa wa urais katika klabu ya Barcelona Victor Font amesema kwamba anafikiria kumrudisha Guardiola iwapo atachaguliwa. Guardiola aliishindia klabu hiyo mataji 14 wakati akiwa mkufunzi wake. Guardiola alikuwa akizungumza baada ya timu yake ya Manchester City kuilaza klabu ya Sheffield United 1-0 katika ligi ya Premia. Ilikuwa mechi ya tatu ya City katika wiki moja baada ya sare na West Ham kufuatiwa na ushindi wa 3-0 dhidi ya Marseille katika kombe la klabu bingwa siku ya Jumanne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako