• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa Macadamia wanataka madalali wafungiwe nje

    (GMT+08:00) 2020-11-03 20:30:24

    Wakulima wa Macadamia huko Meru wanataka serikali iingilie kati na kuwachukulia hatua chama cha wauzaji ambacho kimewatesa, wakisema wamepata udhibiti wa sekta hiyo.

    Madalali walidhibiti sekta hiyo kati ya 2009 wakati usafirishaji wa karanga mbichi ulipigwa marufuku nchini Kenya na 2012, wakinunua karanga hizo kwa chini ya Sh20 kwa kilo.

    bei ya zao hilo iliboreshwa kutoka Sh30 kwa kilo mnamo 2013 hadi mwaka jana wakati wakulima waliuza mazao hayo Sh200 kwa kilo.

    Lakini, tangu kufungwa kwa viwanda kutokana na janga la Corona mapema mwaka huu, bei zimeshuka hadi chini ya Sh40 kwa kilo sasa.

    Wakulima sasa wanashutumu wasindikaji kwa kushirikiana na madalali, ambao wamerudi, kuwanyonya.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Meru Macadamia Joshua Muriira amesema madalali wamechukua soko tena na kumtaka waziri wa Kilimo Peter Munya aingilie kati.

    Amesema wasindikaji walitumia janga la Corona na kutangaza kusitisha ununuzi lakini walikuwa wakipokea mazao kutoka kwa madalali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako