• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amfuta kazi gavana benki kuu bwana Wani katikati ya uchumi uliodorora

    (GMT+08:00) 2020-11-03 20:31:15

    Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir mwanzoni mwa wiki alimfuta kazi gavana wa Benki Kuu Jamal Wani katikati ya Uchumi uliodorora.

    Katika agizo la Rais Bw Kiir alimteua gavana wa zamani Dier Tong kuchukua nafasi ya Bw Wani.

    Rais hakutoa sababu za kumtimua Bw Wani, lakini alitaja nguvu za urais zilizo kwenye Katiba.

    Gavana mpya wa Benki Kuu, Bw Tong, hapo awali alikuwa amehudumu katika nafasi hiyo hiyo kuanzia Mei 2018 hadi Januari mwaka huu wakati Rais Kiir alipomfuta kazi na kumteua Bw Wani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako