• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asema uchumi wa China unatia matumaini na uwezo wa kudumisha maendeleo ya utulivu ya muda mrefu

    (GMT+08:00) 2020-11-03 20:40:43

    Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Xi Jinping amesema uchumi wa China unatia matumaini na unaweza kudumisha maendeleo ya utulivu ya muda mrefu.

    Akitoa hotuba ya ufafanuzi juu ya pendekezo la Kamati Kuu ya CPC kuhusu kuandaa mpango wa 14 wa miaka mitano kwa ajili ya Uchumi wa Taifa na Maendeleo ya Jamii na malengo ya muda mrefu hadi mwaka 2035 ambayo yametangazwa leo, rais Xi amesisitiza kuwa kuna uwezekano kabisa kwa China kufikia viwango vya sasa vya nchi zenye mapato ya juu hadi ifikapo mwishoni mwa kipindi cha 14 cha Mpango wa Miaka Mitano (2021-25) na kuongeza maradufu kiwango cha jumla cha uchumi hadi kufikia mwaka 2035.

    Hata hivyo amesema katika kipindi kijacho kuna mambo mengi yasiyo na uhakika na utulivu kwenye mazingira ya nje ambapo hatari nyingi na zilizojificha zinaweza kuathiri maendeleo ya uchumi wa ndani, akiongeza kuwa janga la COVID-19 limeleta athari kubwa na uchumi wa dunia unaweza kuendelea kuporomoka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako