• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Cote d'lvoire yaonesha rais wa sasa Alassane Outtara amechaguliwa tena

    (GMT+08:00) 2020-11-03 20:41:44

    Rais wa sasa wa Cote d'lvoire Alassane Outtara ameshinda kwenye mbio za uchaguzi uliofanyika Jumamosi kwa kupata zaidi ya asilimia 94 ya kura.

    Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa leo Jumanne na Tume ya Uchaguzi, Outtara amepata kura 3,031,483 na kuchaguliwa kuwa rais tena. Kati ya wapiga kura 6,066,441, tume ya uchaguzi imepata kura halali 3,269,813 kutoka vituo vya kupigia kura 17,601, ambapo wapiga kura waliojitokeza kwenda kupiga kura ni asilimia 53.90

    Wagombea wa upinzani Henri Konan Bedie na Pascal Affi N'Guessan, ambao wote wawili walitoa wito kwa watu kugoma kupiga kura wamepata asilimia 1.66 na 0.99 ya kura mtawalia. Naye mgombea wa kujitegemea Kouadio Konan Bertin amepata asilimia 1.99 ya kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako