• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapiga kura katika uchaguzi wa rais

    (GMT+08:00) 2020-11-04 09:08:49

    Upigaji kura wa uchaguzi mkuu nchini Marekani umeanza, na inakadiriwa kuwa mamilioni ya wapiga kura nchini humo wamejitokeza katika vituo vya kupiga kura kuchagua rais wa awamu ijayo, wabunge na baadhi ya maofisa wa majimbo.

    Takwimu husika zimeonesha kuwa, kutokana na athari ya janga la COVID-19, takriban wapiga kura milioni 100 wa Marekani wakiwemo wagombea wawili wa urais Donald Trump na Joe Biden wamepiga kura mapema au kutumia njia ya posta kupiga kura zao.

    Kutokana na kura zilizopigwa mapema na kutumwa kwa njia posta kuwa nyingi, matokeo ya uchaguzi huo huenda yatachelewa kutangazwa. Vyombo vya habari na raia wana wasiwasi kuwa, huenda migogoro ya jamii itatokea kama mabishano juu ya uchaguzi huo yatatokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako