• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikutano ya Kamati ya sheria na ufundi kuhusu Bwawa la Nile la Ethiopia yamalizika

    (GMT+08:00) 2020-11-04 09:10:28

    Kamati ya sheria na ufundi, inayojumuisha wataalam kutoka Misri, Ethiopia na Sudan, jana imemaliza mikutano yake kuhusu mvutano wa Bwawa la GERD la Ethiopia linalojengwa katika Mto Nile.

    Msemaji wa Wizara ya Rasilimali ya Maji na Umwagiliaji nchini Misri Mohamed al-Sebai amesema, mikutano hiyo ilizungumzia mchakato wa majadiliano yajayo ya ngazi ya mawaziri kuhusu kujaza na majukumu ya Bwawa hilo.

    Wakati huohuo, al-Sebai amesema nchi hizo tatu zitawasilisha maoni yao wakati wa mkutano wa mawaziri wa maji utakaofanyika kesho kwa njia ya video.

    Sudan, Misri na Ethiopia zimefanya majadiliano chini ya uangalizi wa Umoja wa Afrika juu ya masuala ya ufundi na sheria yanayohusiana na kujaza na kazi za Bwawa hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako