• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Uingereza zakamilisha mazungumzo kuhusu biashara baada ya BREXIT

    (GMT+08:00) 2020-11-04 09:10:53

    Kenya na Uingereza zimekamilisha makubaliano ya uhusiano wa kiuchumi (EPA) jana Jumanne, ambayo yatahakikisha urahisi wa biashara wakati Uingereza itakapojitoa kwenye Umoja wa Ulaya Desemba 31 mwaka huu.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na kiongozi wa ujumbe wa Kenya katika mazungumzo hayo, Johnson Weru, ambaye pia ni Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Viwanda na Biashara, na kiongozi wa ujumbe wa Uingereza Paul Waters imesema, pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kimsingi ya Uhusiano wa Kiuchumi kati ya Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Uingereza.

    Taarifa hiyo pia imesema, maofisa wa serikali wa nchi hizo mbili wamesaini waraka huo, ikiashiria kumalizika kwa mazungumzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako