• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya uchaguzi ya Uganda yawapitisha wagombea 11 wa nafasi ya urais kwa uchaguzi wa mwakani

    (GMT+08:00) 2020-11-04 09:11:26

    Tume ya Uchaguzi ya Uganda imemaliza zoezi la siku mbili la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini humo mwaka ujao, na kuwapitisha wagombea 11 wa nafasi hiyo.

    Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Simon Byabakama amesema kwa njia ya televisheni kuwa, wagombea watano wameteuliwa na vyama vya siasa, na wengine tisa ni wagombea huru.

    Wagombea waliopitishwa ni pamoja na rais wa sasa Uganda Yoweri Tibahaburwa Kaguta Museveni, John Katumba, Nancy Kalembe ambaye ni mgombea pekee mwanamke, mwanamuziki maarufu Robert Kyagulanyi Ssentamu, na Fred Mwesigye.

    Jaji Byabakama amewapongeza wagombea waliopitishwa, na kuwataka kuendeleza shughuli zao kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa kwa ajili ya kampeni.

    Pia amewataka wagombea hao kusimamia ushiriki salama katika mchakato wa uchaguzi kwa kufuata hatua zilizowekwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako