• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China katika UM atoa mwito wa kuhimiza amani kwa kupitia maendeleo

    (GMT+08:00) 2020-11-04 09:23:22

    Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun jana kwenye kikao cha ngazi ya juu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu "kujenga amani na kudumisha amani" amesisitiza kuwa, maendeleo ni msingi muhimu wa kutatua masuala yote.

    Balozi Zhang amesema, kutatua migogoro kwa njia ya amani ni moja ya kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa, na inapaswa kupinga kutumia nguvu na kutishia kutumia nguvu katika uhusiano wa kimataifa.

    Amesema, mshikamano na ushirikiano ni silaha yenye nguvu ya kushinda migogoro yote, na nchi mbalimbali zinapaswa kushirikiana na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu. Matishio na changamoto za kimataifa zinahitaji kukabiliana kwa dunia nzima, utaratibu wenye pande nyingi unapaswa kulindwa, na umuhimu wa Umoja wa Mataifa unapaswa kuimarika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako