• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aeleza wasiwasi kuhusu vitendo vya kimabavu nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-11-04 09:26:01
    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aeleza wasiwasi kuhusu vitendo vya kimabavu nchini Ethiopia Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ameeleza wasiwasi kubwa kuhusu mgogoro wa kikabila na mashambulizi dhidi ya raia nchini Ethiopia, ambayo yamesababisha idadi kubwa ya vifo. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric imesema, Bw. Guterres ametoa wito kwa wadau wote kuchukua hatua za haraka kutuliza migogoro nchini humo na kukabiliana changamoto zote kupitia mazungumzo ya amani. Habari nyingine zinasema, shambulizi lingine lilitokea katika jimbo la Oromia na kusababisha vifo vya watu nne na wengine 3 kujeruhiwa. Wahanga walikuwa wanajenga daraja wakati walishambuliwa na watu wenye silaha wa kundi la OLA “Oromo Liberation Army”.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako