• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Hassan Mwakinyo apanda viwango kwa nafasi 14

    (GMT+08:00) 2020-11-04 17:09:16

    Hassan Mwakinyo aliyewahi kuwa namba moja Afrika na wa 14 duniani baada ya kumchapa kwa TKO, Samm Eggington wa Uingereza aliyekuwa bondia namba nane wa dunia kwenye uzani wa Super Welter mwaka 2018, mwanzoni mwa mwaka huu aliporomoka hadi nafasi ya 86 duniani. Amepanda kwa nafasi 14 katika viwango vya ngumi duniani, huku akitajwa kuwa bondia namba moja nchini Tanzania. Kwa mujibu wa viwango vipya vya mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), Mwakinyo sasa ni bondia wa 72 duniani kutoka nafasi ya 86 aliyokuwepo awali kwenye uzani wa super welter anaopigania. Katika ubora wa mabondia wa kila uzani (Pound for Pound), Mwakinyo ameingia kwenye 'top 50' ya Afrika inayoongozwa na Junior Makabu na Richard Commey wanaopigania uzani wa Cruiser raia wa DR Congo na Kevin Lerena anayepigania uzani wa light raia wa Afrika Kusini amehitimisha tatu bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako