• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapata Sh1b kutoka shirika la TMEA kwa ajili ya miradi ya miundombinu

    (GMT+08:00) 2020-11-04 18:06:57

    Serikali ya Kenya imepokea Sh1.3 bilion kutoka Shirika la TradeMark East Africa (TMEA) ili kufadhili miradi ya miundombinu katika kaunti mbili.

    Kaunti ya Busia itapokea sehemu kubwa ya fedha hizo kwa ajili ya miradi mitatu ya miundombinu,ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa soko la mpakani la Jumuiya (Sh485.3 milioni), nayo Mombasa itapata Sh200 milioni kwa ajili ya mradi wa barabra wa mtaa wa Magongo.

    Kituo cha mpakani cha Malaba kitapokea Sh403 million, huku barabara inayoelekea katika kituo hicho ikipokea Sh372 million.

    Akizungumza wakati wa utiaji saini jijini Nairobi jana,Waziri wa Fedha Ukur Yatani alisema ukamilishaji wa miradi utasaidia kuchochea uchumi wa kikanda.

    Yatani alisema msaada huo utasaida kurahisisha biashara na ukuaji wa uchumi wa Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo,baada ya kukamilika kwa kituo cha mpakani cha Malaba.

    Ukamilishaji wa barabara ya Magongo kuelekea bandari ya Mombasa unatajwa kuwa mchango mkubwa katika kupunguza msongamano wa magari barabarani.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Trademark East Africa David Stanton alisema wamejitolea kuboresha miradi miundombinu nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako