• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Uganda yalenga kupanua mtandao wa reli hadi Sudan kusini

    (GMT+08:00) 2020-11-04 18:07:52

    Waziri wa Fedha nchini Uganda Matia Kasaija amesema iwapo fedha zitapatikana,serikali itapanua mtandao wa reli hadi Sudan Kusini.

    Akizungumza wakati wa ukabidhi wa ofisi kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la reli la Uganda ,Kasaija alisema njia nafuu ya uchukuzi,ambayo ni uwekezaji wa reli unafaa kupewa kipaumbele.

    Alisema kuwa ikiwa sasa wanaweza kukarabati reli ya zamani hadi Tororo,na iwapo fedha zitaruhusu watajenga reli hiyo iunganishe hadi Sudan kusini kwa sababu ndio njia rahisi ya uchukuzi.

    Sudan kusini ni sehemu muhimu ya soko la mauzo ya nje ya Uganda baada ya Kenya.

    Mwaka 2019,nchi ya Sudan kusini iliingizia Uganda mapato ya $351.5m.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako