• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia dola milioni moja kwa UNICEF ili kukabiliana na utapiamlo nchini Senegal

    (GMT+08:00) 2020-11-04 19:18:26

    China imechangia dola za kimarekani milioni moja kwa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ili kusaidia watoto wenye utapiamlo mkali nchini Senegal ikiwa kama sehemu ya mwitikio wa janga la COVID-19.

    Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika jana UNICEF ya Senegal imesema janga la COVID-19 limeongeza hatari ya utapiamlo kwa watoto kutokana na chakula kutokuwa bora, ukosefu wa huduma za lishe na nyingine za afya. Mwakilishi wa UNICEF Silvia Donailov ameishukuru China kwa kuhamasisha misaada na kuona umuhimu wa kuunga mkono juhudi zao pamoja na Senegal na kusema mchango huo utasaidia kunusuru watoto.

    Kwa upande wake balozi wa China nchini Senegal Xiao Han amesema China inajivunia kuanzisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa wa kusaidia nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako