• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia kuchukua hatua kusukuma mbele ustawi wa pamoja

    (GMT+08:00) 2020-11-04 19:26:42

    Waraka wa mapendekezo ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kuandaa mpango wa 14 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii na malengo ya maendeleo ya mwaka 2035, umetangazwa jana. Hii ni mara ya kwanza kwa kamati hiyo kusisitiza kusukuma mbele ustawi wa pamoja kwenye waraka wa mkutano wao na kutoa sera kadhaa katika sekta ya usambazaji wa mapato.

    Kwa mujibu wa waraka huo, hadi mwaka 2035, wastani ya pato la taifa la China kwa mtu utakuwa sawasawa na nchi za ngazi ya kati zilizoendelea. Idadi ya watu wenye mapato ya katikati itaongeza na kuwa kubwa. Huduma za kimsingi za umma zitatimiza usawa. Pengo la mapato ya watu wa mijini na vijijini litapungua sana. Maisha ya watu na ustawi wa pamoja wa watu wote vitapata maendeleo halisi makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako