• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UM atoa wito kwa Cote d'Ivoire kudumisha utulivu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais

    (GMT+08:00) 2020-11-04 19:27:10

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa Cote d'Ivoire kudumisha utulivu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais.

    Bw. Guterres amelaani vikali vurugu zilizotokea kabla na baada ya uchaguzi huo. Amezitaka pande zote husika kuheshimu utaratibu wa kikatiba na sheria za nchi hiyo na kufanya mazungumzo jumuishi na ya maana kati yao ili kujitahidi kwa pamoja kufikia makubaliano na mshikamano wa taifa.

    Bw. Guterres pia amesema, Umoja wa Mataifa unapenda kuunga mkono mazungumzo hayo yanayolenga kulinda utulivu na kuhimiza maridhiano nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako