• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya kimataifa ya uagizaji bidhaa nje ya China yatoa fursa ya kufufua uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-11-05 09:23:34

    Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wamesema kuwa, Maonyesho ya tatu ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China (CIIE) ni zoezi la kufungua nafasi mpya kwa maendeleo ya dunia na kutoa fursa kwa dunia, na pia yatatia nguvu katika biashara ya kimataifa na uchumi.

    Wakizungumza katika ufunguzi wa maonyesho hayo kwa njia ya video, viongozi hao wameisifu China kwa mafanikio yake katika kukabiliana na changamoto zilizotokana na janga la virusi vya Corona na kufanya maonyesho hayo kama ilivyopangwa awali.

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemshukuru rais Xi Jinping wa China na wananchi wake kwa kushinda changamoto na kufanya maonesho hayo kama ilivyopangwa. Amesema kutangaza biashara na fursa za uwekezaji ni muhimu sana kwa ajili ya hali ya sasa ya kufufuka kwa uchumi. Pia amesema, China ni mwenzi wa muda mrefu wa biashara wa Afrika, na maonesho hayo yanatoa jukwaa muhimu kwa nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako