• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya usimamizi wa amani yasema majadiliano yanayoendelea ni muhimu kwa amani ya kudumu nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-11-05 09:24:03

    Mkuu wa Tume Mpya ya Pamoja ya Usimamizi na Tathmini (RJMEC) Berhanu Kebede amesema, majadiliano ya kitaifa yanayoendelea katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, yanayozikutanisha jamii mbalimbali pamoja kuzungumzia amani na upatanishi yatatoa suluhisho la kutimiza amani ya kudumu nchini humo.

    Bw. Kebede amesema, mapendekezo yatakayofikiwa mwisho wa mkutano huo yatakuwa na maslahi muhimu katika mchakato wa utekelezaji wa makubaliano ya amani ambao bado haujaanza.

    Pia matokeo ya mkutano huo yatasaidia katika utekelezaji wa Kifungu cha Tano cha makubaliano ya amani kinachopendekeza kuwa na mpito wa sheria baada ya zaidi ya miaka sita ya mapigano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako