• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kulinda usalama wa askari polisi wa kulinda amani

    (GMT+08:00) 2020-11-05 09:24:06

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun jana kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu askari polisi wa kulinda amani, ametoa wito wa kuhakikisha usalama wa askari hao, na kuimarisha ujenzi wa uwezo wao.

    Balozi Zhang amesema, askari hao wanakabiliwa na hatari kubwa, na kuhakikisha usalama wao ni sharti la kwanza kwao kutekeleza majukumu yao. Amesema nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na Sekretarieti ya Umoja huo zitatakiwa kuchukua hatua ili kuwasaidia askari polisi hao kuongeza uwezo wao wa kutambua hatari mapema, kuboresha vifaa vyao vya kazi na kuongeza kiwango cha matibabu, na kupunguza hatari ya usalama hadi kiwango cha chini zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako