• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atatoa pendekezo gani katika mkutano wa 20 wa baraza la wakuu wa SCO?

    (GMT+08:00) 2020-11-05 15:46:44

    Rais Xi Jinping wa China tarehe 10 Novemba atashiriki na kuhutubia mkutano wa 20 wa baraza la wakuu wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai SCO kwa njia ya video. Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Le Yucheng amesema, rais Xi na viongozi wengine watakaoshiriki kwenye mkutano huo watajadili wazo jipya na hatua mpya za ushirikiano katika kukukabiliana na changamoto na hatari, na kuhimiza usalama, utulivu, maendeleo na ustawi, na kutoa mapendekezo kadhaa ya kuhimiza maendeleo tulivu ya shirika hilo katika muda huu wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Bw. Le Yucheng amesema hii ni mara ya kwanza kwa rais Xi kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa mashirika ya pande nyingi baada ya mkutano wa 5 wa wajumbe wote wa awamu ya 19 ya chama cha kikomunisti cha China, pia ni shughuli muhimu ya kidiplomasia ya China kwa sehemu za Ulaya na Asia, ambayo ina umuhimu mkubwa. Anasema,

    "pande mbalimbali zitabadilishana maoni kuhusu namna ya kuimarisha kazi zinazopewa kipaumbele za Shirika la Ushirikiano la Shanghai, na masuala makubwa ya kikanda na ya kimataifa katika hali ya maambukizi ya virusi vya Corona. Nchi za shirika hilo kufanya mkutano huo kwa njia ya video kunaonyesha kuwa pande mbalimbali zinatilia maanani sana maendeleo ya shirika hilo, na nia ya thabiti ya kuendelea kueneza moyo wa Shanghai, kushirikiana kukabiliana changamoto za hatari na kulinda kwa pamoja usalama wa taifa na maslahi ya maendeleo ya kanda hiyo. "

    Bw. Le Yucheng amefahamisha kuwa, licha ya viongozi wa nchi 8 wanachama wa shirika hilo, viongozi wengine wa nchi waangalizi wanne pamoja na wajumbe wa jumuiya za kimataifa pia watashiriki kwenye mkutano huo. Rais Xi Jinping wa China pamoja na viongozi hao watajadili wazo jipya na hatua mpya za kiushirikiano katika kukabiliana na changamoto na hatari, na kuhimiza usalama, utulivu, maendeleo na ustawi. Anasema,

    "kwenye hotuba yake, rais Xi atatoa mapendekezo na utetezi kadhaa kuhusu kuendelea kueneza moyo wa Shanghai, kuimarisha mshikamano na hali ya kuaminiana ya shirika hilo, kuzidisha ushirikiano wa sekta mbalimbali, kuimarisha muungano kati ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mkakati wa maendeleo wa nchi mbalimbali pamoja na ushirikiano wa kikanda, kuunga mkono hali ya pande nyingi, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu, ili kuhimiza maendeleo tulivu na ya muda mrefu ya shirika hilo katika muda huu wa maambukizi ya virusi vya Corona."

    Habari zinasema katika mkutano huo viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo watatoa azimio la mkutano, na kupitisha nyaraka za ushirikiano katika sekta mbalimbali. Bw. Le Yucheng amesema, China inatarajia pande mbalimbali zitatumia fursa hii kufikia hatua mpya za ushirikiano, na kutia motisha wenye nguvu kwa maendeleo na ustawi wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako