• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia yatoa wito wa kuboresha utengezaji ili iweze kuwepo kwenye biashara ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-11-05 18:53:31

    Waziri wa Viwanda na Biashara wa Namibia Lucia lipumbu leo amesititiza umuhimu wa nchi yake kuboresha utengenezaji na kuunda mnyororo wa thamani kama nchi hiyo bado inataka kubaki kwenye biashara iliyoboreka ya Afrika.

    Amesema kuboresha utengenezaji na kuunda mnyororo wa thamani pia kutapiga jeki upatikanaji wa nafasi za ajira pamoja na kuifanya nchi inufaike na uhusiano unaotarajiwa kuboreka wa kibiashara kati ya nchi za Afrika katika siku za karibuni kutokana na Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA. Waziri huyo pia ametoa wito kwa nchi za Afrika kuendeleza utekelezaji wa AfCFTA katika njia ya kutoa na kuokoa nafasi za ajira katika bara zaima la Afrika pamoja na nchi moja moja.

    Kwa mujibu wa Lipumbu, Namibia hivi sasa inashughulikia mpango wa jinsi ya kutekeleza kwa ukamilifu AfCFTA katika kipindi kifupi iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako