• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya kuzalisha zaidi kawi ya jotoardhi

    (GMT+08:00) 2020-11-05 19:22:02

    Wizara ya kawi nchini kenya imesema itaimarisha utafutaji wa rasilimali zaidi ya nishati ya jotoardhi.

    Kwa sasa wizara hiyo inafanya uchunguzi katika maeneo 11 na inaendelea kuchimba visima vitatu vipya vya jotoardhi ili kuzalisha megawati 760 zaidi ya umeme.

    Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (GDC)Jared Otieno, amesema pia ujenzi wa kiwanda cha umeme katika eneo la Nakuru unaendelea.

    Kenya hivi sasa inazalisha umeme wa jotoardhi wa megawati 870 ambazo zinachangia asilimia 40 ya jumla ya uzalishaji wa umeme nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako