• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli wa Tanzania aapishwa kutumikia kipindi cha pili

    (GMT+08:00) 2020-11-05 19:29:57

    Rais wa Tanzania aliyechaguliwa tena John Magufuli ameapishwa leo kutumikia kipindi cha pili cha miaka mitano.

    Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma alimwapisha Magufuli kama rais na mama Samia Suluhu Hassan kama Makamu wa rais katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kwenye sherehe iliyohudhuriwa na viongozi na wawakilishi kutoka nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa.

    Baada ya kula kiapo Magufuli alitoa hotuba akiwataka Watanzania wote kushirikiana pamoja bila kujali kabila, dini, siasa au imani zao ili kuifanya Tanzania iwe nchi inayojitegemea kiuchumi. Pia ametoa wito wa kulinda maliasili za nchi, yakiwemo madini, rasilimali za bahari, wanyamapori na mifugo kwa faida ya Watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako