• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wasema kuendelea kuunga mkono Mkataba wa Paris

    (GMT+08:00) 2020-11-05 19:36:46

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Dujarric jana alisema, hapo awali Mkataba wa Mwongozo wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Tabia nchi UNFCCC na baadhi ya nchi zilitoa taarifa zikisema, kulinda dunia na binadamu na kuepuka mabadiliko ya hali ya hewa ni kazi muhimu sana, Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono mkataba wa Paris.

    Msemaji huyo alisema kuwa, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ataongoza mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia nchi tarehe 12 mwezi Disemba wakati wa kuadhimisha miaka 5 tangu kusainiwa kwa mkataba wa Paris, na kusisitiza kuwa uungaji mkono na nia ya Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa Paris hautabadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako