• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wa Falme za Kiarabu na Bahrain wapigwa chanjo ya COVID-19 ya China

    (GMT+08:00) 2020-11-05 19:37:15

    Habari kutoka vyombo vya habari vya nchi za nje zinasema, Makamu wa rais ambaye pia ni waziri mkuu wa Flame za Kiarabu na mtawala wa Dubai Mohammed bin Rashid Al Maktoum alisema kuwa amepigwa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China.

    Habari zinasema kuwa, chanjo hiyo ilichunguzwa na kampuni ya Sinopharm, hivi sasa ipo kwenye kipindi cha tatu cha majaribio ya hospitalini. Vyombo vya habri vilinukuu habari kutoka serikali ya Falme za Kiarabu ikisema kuwa, chanjo hiyo ni salama na yenye ufanisi. Kabla ya Bw. Al Maktoum kupigwa chanjo hiyo, maofisa 10 wa nchi hiyo walipigwa chanjo hiyo. Aidha madaktari na wauguzi wa nchi hiyo pia watapigwa chanjo hiyo.

    Habari nyingine zinasema, Bahrain imeidhinisha wafanyakazi wanaoshughulikia kudhibiti janga la COVID-19 wapigwe chanjo haraka yaCOVID-19 kutoka China kuanzia tarehe 3 mwezi Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako