• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yasema zaidi ya Waafrika milioni 600 wanakosa umeme licha ya uwepo wa nishati mbadala

    (GMT+08:00) 2020-11-06 09:04:00

    Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) imesema kuwa zaidi ya watu milioni 600 barani Afrika wanakosa umeme, licha ya bara hilo kuwa ni hifadhi kubwa ya nishati mbadala.

    Akizungumza katika mkutano wa Geothermal Rift (ARGe-C8) uliofanyika kwa njia ya video, Kamishna wa Miundombinu na Nishati wa Umoja huo Amani Abou-Zeid amesema watu wengi bado wanategemea nishati asilia kama kuni kwa ajili ya kupikia.

    Amesema hatua hiyo inaleta athari kubwa katika juhudi za kuondoa umasikini na maendeleo ya watu katika bara hilo, na kusisitiza kuwa, kuendeleza nishati inayotumia joto kutoka ardhini ni moja ya maeneo yanayozingatiwa na Kamati ya Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako