• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji wa al-Shabaab waharibu mnara wa mawasiliano katika shambulizi kwenye mpaka wa Kenya

    (GMT+08:00) 2020-11-06 09:04:25

    Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wamefanya shambulizi katika eneo la Karo, Mandera, kaskazini mashariki mwa mpaka wa Kenya na kuharibu mnara wa mawasiliano, hivyo kuathiri mawasiliano katika eneo hilo.

    Mkuu wa Kaunti ya Mandera, Onesmus Kyatha amesema, shambulizi hilo lililotokea Jumatano usiku ni la karibuni zaidi linalolenga minara ya mawasiliano, na kuongeza kuwa vikosi vya usalama vinawasaka wapiganaji waliofanya shambulizi hilo.

    Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wamekuwa wakilenga minara ya mawasiliano, shule, na nyumba zilizokodishwa na watu ambao sio wakazi wa kaunti za Garissa, Mandera na Wajir zilizoko kaskazini mashariki mwa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako