• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 9 wa baraza la jumuiya za washauri bingwa kati ya China na Afrika wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2020-11-06 09:32:21

    Mkutano wa 9 wa baraza la jumuiya za washauri bingwa kati ya China na Afrika umefunguliwa hapa Beijing, ukishirikisha wawakilishi wa pande mbili, wakiwa ni pamoja na viongozi wastaafu, viongozi waandamizi, wanadiplomasia na wanahabari kutoka China na Afrika. Mkutano huo umehusisha washiriki waliojumuika hapa Beijing na wengine walioshiriki kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kwa njia ya mtandao wa Internet.

    Mkutano huu ambao ni sehemu ya shughuli za baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, umefanyika chini ya kauli mbiu ya "kuangalia yaliyofanyika na kuangalia matarajio" kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuangalia mchango wa jumuiya za washauri bingwa za pande mbili kwenye kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika. Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano huo msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Deng Li amekumbusha umuhimu wa baraza la ushirikiano kati ya China na hasa umuhimu wa jumuiya za washauri bingwa kwenye uhusiano kati ya China na Afrika.

    Anasema, "Jumuiya za washauri bingwa za China na Afrika zinatakiwa kufuatilia vizuri hali ya sasa ya kimataifa, na kuangalia uhusiano kati ya China na Afrika kwa upeo wa kimataifa na kimaendeleo. Pia zinatakiwa kufanya ukaguzi na utafiti kwa jamii, ili wawe wataalamu wa pekee kwenye sekta maalumu. Natoa mwito washauri bingwa waeleze vizuri mambo kati ya China na Afrika, pia wanapaswa kutoa maoni sahihi yanayolingana na hali halisi wakati tunaposhambuliwa kwa maneno na watu wa nje, ili kuwaongoza watu waelewe vizuri uhusiano kati ya China na Afrika kwa kulingana na hali halisi na kwa haki".

    Bw. Deng Li pia amelitaja baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika kuwa ni jukwaa muhimu la mfano wa ushirikiano wa Kusini-Kusini, linalozingatia kanuni tano za kuishi pamoja kwa masikilizano, na limeleta miradi ya yenye mafanikio kwa pande zote kutokana na uchapaji kazi wa watu wa pande mbili. Washiriki wa mkutano huo pia wameona haja zaidi ya kutumia jumuiya za washauri bingwa kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.

    Aliyekuwa rais wa Msumbiji Bw. Joachim Chissano amesema ushirikiano katika ngazi ya serikali ni mzuri lakini kuna changamoto kwenye ushirikiano kati ya watu na watu wa pande hizo mbili, jumuiya za washauri bingwa zinaweza kuimarisha ushirikiano katika eneo hilo, na kupendekeza maeneo zaidi ya ushirikiano kutokana na tafiti zinazofanywa, anasema, "ni kweli uhusiano kati ya China na Afrika umeimarika sana, na bado unaendelea kuimarika. Hata hivyo kuimarika huko kuko zaidi kwenye ngazi ya serikali. Ili kuimarisha zaidi ushirikiano wetu, tunatakiwa kupanua maeneo ya ushirikiano, na kufanya ushirikiano wetu uwe shirikishi zaidi na jumuishi, kwa kuimarisha mafungamano ya watu wa kawaida. Hali hii sio tu itatoa uhalali wa maamuzi yanayofanywa, na njia za ushirikiano zinazochaguliwa, lakini pia itawafanya watu waone wanaumiliki ushirikiano huu".

     Mbali na hayo Bw. Chissano amesema jumuiya za washauri bingwa pia zinatakiwa kuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vinavyo upaka matope uhusiano kati ya China na Afrika. Kiongozi wa mabalozi wa nchi za Afrika nchini China, ambaye pia ni balozi wa Cameroon nchini China Bw, Martin Mpana amesema jumuiya za washauri bingwa ni wazo zuri lakini bado zina kazi nyingi za kufanya.

    Bw. Mpana anasema, "Bado kuna kazi nyingi za kufanya, tunahitaji kuwekeza muda zaidi na nguvu kazi zaidi kwenye utafiti, ili tuweze kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye uhusiano wetu, hilo ndio jukumu la jumuiya za washauri mbili. Hili ni wazo zuri sana, kwani hatutakiwi kujadili uhusiano wetu kwenye majukwaa ya kidiplomasia tu, tunatakiwa kuzungumzia mahusiano yetu kwenye vyuo vikuu, kwenye mambo ya sayansi na teknolojia na hata kwenye mambo ya utafiti. Tukifanya hivyo ndio tunaweza kuimarisha mahusiano yetu kwa kina, na kuweza kuongeza mambo yetu kwa sauti moja. Kwa hiyo naona lilikuwa pendekezo zuri, ni bora tukawapa nafasi ya kufanya kazi, na kutoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha mahusiano yetu".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako