• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya usambazaji umeme kuongeza bei Ya Stima  Kenya

    (GMT+08:00) 2020-11-06 16:42:40

    Gharama ya maisha nchini Kenya inatarajiwa kupanda kufuatia mpango wa kampuni ya usambazaji umeme, Kenya Power, wa kutaka kuongeza bei ya umeme.

    Duru kutoka mamlaka ya kusimamia sekta ya kawi nchini Kenya (EPRA) zinasema imeidhinisha ombi la kampuni hiyo la kutaka kuongeza bei ya umeme kwa hadi kiwango cha asilimia 20.

    Inakisiwa kuwa hiyo ni sehemu ya mpango wa Kenya Power wa kujinasua kutokana na changamoto za kifedha, kiasi kwamba kampuni hiyo inabanwa na mzigo wa bei wa kununua umeme kutoka kwa wazalishaji kawi hiyo.

    Ikiwa nyongeza hiyo itatekelezwa, ada za umeme zitaongeza mzigo kwa familia ambazo zinabanwa na mzigo wa kiuchumi unaotokana na janga la Covid-19.

    Watengenezaji bidhaa na wafanyabiashara wengine pia watabebeshwa mzigo wa nyongeza ya gharama ya uzalishaji.

    Hata hivyo, kabla ya nyongeza hii kutekelezwa pendekezo hilo ni lazima liwasilishwe kwa wananchi ili watoe michango, maoni na mapendekezo yao.

    Kampuni ya Kenya Power ilikuwa imewasilisha ombi la kutaka bei ya umeme kuongezwa mnamo 2019 ambapo tume ya EPRA ilikubali pendekezo hilo. Hata hivyo, utekelezaji wa ombi hilo ulisitishwa kwa muda kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.

    Kufuatia nyongeza hizo wateja wanaotumia umeme wa kiasi cha kilowati 100 kila mwezi watalipa Sh12.50 kwa kila kipimo kutoka ada ya sasa ya Sh10 kwa kila kipimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako