• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja na ndugu zake wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-11-06 18:50:34

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, bila kujali tunakabiliwa na changamoto gani, China itashikamana na kushirikiana na ndugu zake wa Afrika, na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya pande hizo mbili.

    Wang amesema hivi karibuni dawa na vifaa vya matibabu vilivyofadhiliwa na serikali ya China kwa wanawake, watoto na vijana wa Afrika vyote vimefikishwa, na kugawanya na kutumiwa katika nchi 53 za Afrika.

    Amesema tangu kutokea kwa mlipuko wa janga la COVID-19, China na nchi za Afrika zimesaidiana na kuungana mkono. Wakati China inapokabiliana na maambukizi ya virusi nchini, imetoa misaada ya dawa na vifaa vya matibabu vinayohitajika zaidi na nchi za Afrika. Licha ya hayo, China imetuma vikundi vya madaktari na wataalam wa afya kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na janga hilo, na kuahidi kutoa chanjo ya virusi vya corona itakapokamilika kwa nchi zinazoendelea haswa Afrika kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako