• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2020-11-06 18:57:57

    Kamati ya Umoja wa Ulaya jana ilitoa makadirio ya uchumi ikisema, mchakato wa kufufuka kwa uchumi wa Ulaya ulizuiliwa na wimbi la pili la janga la COVID-19, na kamati hiyo ililazimika kupunguza makadirio ya ongezeko la uchumi la mwaka kesho.

    Mjumbe wa kamati hiyo anayeshughulikia mambo ya uchumi Bw. Paolo Gentiloni katika mkutano na waandishi wa habari amesema, uchumi wa Umoja wa Ulaya na uchumi wa eneo linalotumia fedha za EURO utapungua kwa asilimia 7.4 na asilimia 7.8 mtawalia katika mwaka 2020, na kuongezeka kwa asilimia 4.1 na asilimia 4.2 mtawalia katika mwaka 2021.

    Bw. Gentiloni amesema, janga la COVID-19 lilisambaa barani Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, na kusababisha kuporomoka kwa uchumi. Kutokana na kupunguza hatua za vikwazo dhidi ya janga hilo, uchumi wake ulifufuka katika robo ya tatu ya mwaka huu. Lakini kutokana na kurudi tena kwa janga hilo, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zililazimika kuchukua hatua za vikwazo tena na mchakato wa kufufuka kwa uchumi wa Ulaya ulizuiliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako