• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa benki ya Afrika Kusini asema maonesho ya CIIE kusaidia wafanyabishara kuingiliana na kufufua uchumi

    (GMT+08:00) 2020-11-06 19:24:01

    Mkuu wa Benki ya Standard ya Afrika Kusini Philip Myburgh amesema Maonesho ya tatu ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China CIIE yatawawezesha wafanyabiashara wa Afrika na watengezaji wa China kuingiliana na kufikia makubaliano ya kibiashara, ambayo yatasaidia kufufua uchumi wa Afrika baada ya janga la virusi vya corona.

    Amesema maonesho hayo yamekuja wakati ambao uwezeshaji wa kibiashara ni muhimu ili kuondoa athari za kiuchumi zinazotokana na COVID-19, na kwamba wafanyabiashara wa Afrika wanatafuta fursa ya vyanzo mbalimbali na kuondoa hasara waliyoipata katika mwaka huu. Wakati huohuo waagizaji wa bidhaa wa China wanafikiria masoko mapya ya kupata bidhaa kutoka Afrika. Hivyo amesisitiza ni muhimu kutafuta njia mpya za kuwaunganisha wateja wao na masoko yenye uwezo ya wafanyabiashara wa Afika ili kupanuka na kukua zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako