• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uagizaji wa huduma wa China kutoka nchi za nje kufikia dola za kimarekani trilioni 2.5 katika miaka michache ijayo

    (GMT+08:00) 2020-11-06 19:24:34

    Wizara ya biashara ya China imetoa ripoti ikisema uagizaji wa huduma wa China kutoka nchi za nje unatarajiwa kufikia dola za kimarekani trilioni 2.5 katika miaka mitano ijayo, wakati ambao nchi inaendelea kufungua soko lake kubwa.

    Ripoti hiyo inayohusu huduma za uagizaji za China iliyotolewa leo pembeni mwa maonesho ya tatu yanayoendelea huko Shanghai, China, imesema kiasi hicho kitakuwa sawa na asilimia 10 ya uagizaji wa jumla duniani. Pia imesema matumizi ya safari za nje huenda yakazidi dola za kimarekani trilioni 1 katika kipindi hiki, huku uagizaji wa huduma za kidijitali, zikiwemo malipo ya matumizi ya mali za ubunifu na huduma za kifedha, yanaweza kufikia dola trilioni 1.3 za kimarekani.

    Aidha ripoti imebainisha kuwa China italegeza vizuizi vya hisa za kigeni katika ongezeko la thamani la huduma ya mawasiliano ya simu, utamaduni, fedha na biashara kwenye mtandao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako