• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Imam wa msikiti mkoani Xinjiang, China alaani vyombo vya habari vya magharibi kwa kusema China inaangamiza dini ya kiislamu

    (GMT+08:00) 2020-11-06 19:57:50

    Imam wa msikiti wa Oshakand mkoani Xinjiang Bw. Esbiton Saimahdi amesema, vyombo vya habari vya nchi za magharibi kusema serikali ya China inaangamiza dini ya kiislamu na kuwakamata wafuasi wa dini si jambo la kweli.

    Bw. Saimahdi amesema, wale waliokamatwa si wafuasi wa dini bali ni wahalifu wanaojaribu kueneza msimamo mkali, kufarakanisha nchi na kufanya shughuli za kimabavu chini ya bendera ya Uislamu.

    Bw. Saimahdi pia amesema, China ni nchi yenye utawala wa sheria. Serikali ina haki ya kupambana na uhalifu kwa kufuata sheria hasa uhalifu unaohusisha mambo ya kidini. Mapambano dhidi ya msimamo mkali ni njia bora ya kulinda dini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako