• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Afrika wampongeza Biden baada ya kura kuonyesha ameshinda uchaguzi

    (GMT+08:00) 2020-11-09 09:29:21

    Viongozi mbalimbali wa Afrika wametuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Marekani Joe Biden baada ya vyombo vya habari vya nchi hiyo kutangaza kwamba mgombea huyo wa chama cha Democratic ameshinda uchaguzi siku ya Jumamosi.

    Akitoa pongezi zake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Wamerekani wamepaza sauti na kutumia kura zao kumchagua kiongozi mwenye uzoefu wa muda mrefu kuongoza nchi.

    Kwa upande wake rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuchaguliwa kwake ni ukumbusho kwamba demokrasia ndio mfumo mzuri wa serikali kwasababu unawapa watu fursa ya kubadili serikali yao kwa njia ya amani.

    Naye rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewapongeza rais mteule Joe Biden na makamu wa rais Kamala Harris pamoja na Wamerekani, na kusema anatarajia kushirikiana nao na kuimarisha urafiki wao.

    Wakati huohuo rais wa Namibia alisema wakati wa mapambano ya kutafuta uhuru, walimfahamu Joe Biden kama seneta anayepinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na katika kanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako