• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya misaada yatoa wito wa kukabiliana na njaa kali katika nchi nne

    (GMT+08:00) 2020-11-09 09:29:47

    Mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yamesema watu waliopo katika nchi nne zenye uhaba wa chakula zikiwemo Burkina Faso, kaskazini mashariki mwa Nigeria, Sudan Kusini na Yemen wanahitaji msaada haraka ili kuepusha kuingia kwenye njaa kali.

    Akiongea kwenye mkutano na wanahabari mjini Geneva mshauri mwandamizi wa usalama wa chakula katika Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP Claudia Ah Poe amesema wana wasiwasi kwamba wanaweza kukabiliwa na hatari kubwa ya njaa kama hali itakuwa mbaya zaidi katika miezi ijayo. Katika tahadhari iliyotolewa kwa pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo FAO, na WFP pia imeonya kwamba nchi nyingine 16 zitakabiliwa na dharura kubwa ya chakula katika miezi mitatu au sita ijayo.

    Sababu ya misukosuko hii ya kibinadamu ni pamoja na migogoro ya muda mrefu na ukosefu wa ufikiaji wa misaada ya kibinadamu kwenye jamii zenye mahitaji, pamoja na kuporomoka kwa uchumi kutokana na janga la COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako