• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Ethiopia asema operesheni za kijeshi zinalenga kumaliza hali ya kuepuka adhabu

    (GMT+08:00) 2020-11-09 09:38:32

    Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesisitiza kwamba operesheni za kijeshi zinazoendelea katika mkoa wa kaskazini wa Tigray nchini Ethiopia zinalenga kumaliza hali ya kuepuka adhabu, na kusema kwamba hakuna serikali wala katiba inayoweza kuvumilia vitendo hivyo vya kuvunja sheria.

    Pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuelewa mazingira ya kuendelea kutokea kwa ukiukaji wa kundi la TPLF, ambalo limepelekea serikali kuu kuendesha operesheni hii yenye lengo la kumaliza kabisa vitendo hivyo pamoja na nguvu zenye dhamira ya kuleta hali ya taharuki nchini.

    Tangu Jumatano mapema serikali ya Ethiopia imekuwa ikifanya operesheni za kijeshi dhidi ya TPLF, chama tawala katika mkoa wa Tigray na sasa kipo kwenye vita rasmi dhidi ya serikali kuu baada ya TPLF kuripotiwa kushambulia kamandi ya Kaskazini ya Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako